Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

kipa wa Mali atua Yanga

Mali Pic Data Golikipa anaedhaniwa kusajiliwa na Yanga, Diarra Djigui

Sun, 8 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Sahau kuhusu matokeo ya aibu iliyopata jana kwenye mechi yao ya mwisho ya michuano ya Kombe la Kagame, unaambiwa Yanga inaendelea kushusha watu na sasa inafanya mambo yao kimyakimya baada ya jana mchana kweupee kumshusha kipa wao mpya wa kigeni.

Kipa huyo, Diarra Djigui anayetokea Mali na anatajwa kuja kuongeza uimara katika eneo la kulinda lango.

Taarifa zinasema ujio wake uliwalazimu matajiri wa Yanga, GSM kuweka mkazo mkubwa kutokana na kipa huyo kuwa na ofa mbili za kwenda kufanya kazi nchini Afrika Kusini.

Akili ambayo wasaidizi wa Bilionea wa Yanga, Ghalib Mohammed waliyoitumia ni kumleta mapema meneja wa mchezaji huyo akitokea Guinea na kumficha jijini Dar kuzuia mazungumzo yake na klabu zingine hatua ambayo walifanikiwa.

Baada ya kumleta meneja huyo kisha kupatana naye karibu kila kitu kazi ya pili na ya mwisho kwa Yanga iliyosalia ni kumleta Djigui na jana mpango huo ukakamilika akitokea kwao Mali.

Ujio wa Djigui ambaye leo atasaini mkataba wa miaka miwili una maana sasa Yanga wakati wowote wanaweza kuachana na kipa Mkenya Faruk Shikhalo.

Djigui anakuja kufanya kazi na makipa wazawa Erick Johora ambaye juzi jioni Yanga ilimsainisha mkataba, lakini chini yao atakuwa kinda Ramadhan Kabwili.

Kipa huyo wa mali mwenye mwili jumba anakuwa mchezaji wa saba mpya kunaswa na mabingwa hao wa kihistoria nchini baada ya mabeki wa Djuma Shaban kutoka DR Congo, David Bryson aliyekuwa KMC, winga Dickson Ambundo kutoka Dodoma Jiji, kipa Johora aliyekuwa Burundi na washambuliaji kutoka DR Congo, Heritier Makambo na Fiston Mayele.

Kipa huyo aliyezaliwa Februari 27, 1995 ikiwa na maana kwa sasa ana umri wa miaka 26 alikuwa akiidakia Stade Malien ya kwao Mali, pia akiichezea timu ya taifa ya Mali tangu 2015 akianzia zile za Vijana.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz