Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zwane: Nawaza mabao tu

Screenshot 20240122 144332 Zwane: Nawaza mabao tu

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Themba Zwane amesema staili yake ya uchezaji ndiyo inayomfanya ahusike katika mabao.

Zwane alifunga mabao mawili katika ushindi mnono wa Bafana Bafana wa 4-0 dhidi ya Namibia juzi na hivyo kumfanya staa huyo wa klabu ya Mamelodi Sundowns kushinda tuzo Nyota wa Mchezo kwenye Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly.

“Kila mechi, naingia kwa kujiamini nitafunga mabao. Wachezaji wa eneo la ushambuliaji wanapaswa kufunga, na nina furaha kufunga na kushinda tuzo hii. Ina maana kubwa sana kwangu kushinda tuzo ya Nyota wa Mchezo na nina furaha sana kupata ushindi leo (juzi),” alisema Zwane anayezungumza kwa upole.

Akizungumzia mechi yao ijayo, Zwane anasema watawachimba kwa undani Tunisia kujua wanavyocheza na kupanga mbinu za kuwazamisha miamba hao wa Afrika Kaskazini.

“Tunatambua kwamba ngoma haijaisha bado. Itakuwa mechi ngumu sana dhidi ya Tunisia. Tutawasoma vyema na kuja na mpangokazi. Tunatambua kwamba tunapaswa tushinde mechi hii ili tufuzu,” alisema kiungo huyo wa Afrika Kusini.

Ushindi uliipandisha Afrika Kusini hadi nafasi ya pili nyuma ya Mali ya kipa wa Yanga, Djigui Diarra, kuelekea mechi yao dhidi ya Tunisia kesho. Tunisia wako mkiani wakiwa na pointi moja.

Chanzo: Mwanaspoti