Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zuberi Katwila: Wachezaji wana matatizo ya kisaikolojia

Zuberi Katwila Mtibwa.png Kocha Mkuu Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila.

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema kuwa wachezaji wake wana matatizo ya kisaikolojia ndiyo maana timu yake inapata matokeo mabovu.

Katwila amesema hayo baada ya timu yake kupoteza kwa bao 1-0 mbele ya KMC na kuendelea kusalia mkiani mwa Ligi Kuu wakiwa na alama 17 pekee.

"Ni wazi tunapaswa kufanyia kazi upande wa saikolojia za wachezaji wetu ili waweze kurejesha hali yao ya kujiamini na kuipambania timu kubaki ligi kuu msimu ujao.

"Nina uhakika kama wanaweza kutuliza akili na kuweka mkazo kwenye mechi zijazo, tunaweza kukusanya pointi za kutosha zitakazotusaidia kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

"Kama Kocha Mkuu naamini tuna nafasi ya kusalia kwenye ligi msimu ujao lakini lazima tuhakikishe saikolojia za wachezaji wetu ziko vizuri," amesema Zuberi Katwila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live