Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zubaeni tu, wanachukua hawa

GOAL   Blank WEB   Facebook (1) Wachezaji wa Arsenal wakishangilia goli la ushindi dhidi ya Bournemouth

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa soka Chris Sutton amesisitiza hakuna timu yenye uwezo wa kuipiku Arsenal kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Kuu England msimu huu.

Mkongwe huyo aliyewahi kukipiga Aston Villa na Birmingham City akaongeza akadai Arsenal ndio mabingwa wa ligi baada ya ushindi mkubwa waliopata wa mabao 3-2 dhidi ya Bournemouth wikiendi iliyopita.

Arsenal almanusura ipoteze pointi kwenye mchezo huo lakini kutokana na ubora wao wachezaji wa Mikel Arteta wakapindua meza na kuibuka na ushindi dhidi ya Bournemouth.

Matumaini ya Arsenal kwenye kinyang'anyiro cha mbio za ubingwa yalikatika ghafla baada Bournemouth kupata bao la kuongoza dakika ya kwanza tu ya mtanange huo.

Hata hivyo Arsenal ikapambana na kusawazisha mabao yao kupitia Thomas Partey na Ben White baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0, kabla ya Reiss Nelson kuishindilia Bournemouth dakika ya 97 kabla ya kipenga kupulizwa.

Mkongwe wa soka Sutton akawapongeza Arsenal kutokana na upambaji iliyosababisha wao kuibuka na ushindi muhimu, Arsenal ikiendelea kukaa kileleni kwa tofauti ya pointi tano kwenye msimamo wa ligi dhidi ya Manchester City.

Sutton aliandika kupitia ukurasa wake wa twitter "Nadhani huu ni msimu wa Arsenal, matokeo mazuri sana, ushindi mkubwa wameupata, vile vile mechi ilibadilishwa na Reiss Nelson,"

Wakati huo huo fowadi wa Arsenal, Eddie Nketiah akamsimfia Nelson kupitia ukurusa wake wa twitter kutokana na bao lake alilofunga dakika ya 97 ya mchezo huo "Reis Nelson mpambanaji, amebadilisha matokeo,"

Nao mashabiki wa Arsenal wakashindwa kujizuia hisia zao kutokana na ushindi waliopata wakidai msimu huu wana jambo lao.

Shabiki mmoja wa Arsenal akaandika komenti "Arsenal imejipanga msimu huu watateba ubingwa wa ligi" mwingine akaandika " Arsenal itabeba ubingwa, wameonyesha kitu kusawazisha mabao matatu sio mchezo,"

Baada ya mchezo huo Arsenal itasafiri kuelekea Ureno kwaajili ya mechi yao ya Ligi ya Europa raundi ya 16 bora dhidi ya Sporting Lisbon, kabla ya kurejea jijini London kwaajili ya mchezo wao mwingine wa ligi dhidi ya Fulham.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live