Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zoran humwambii kitu kwa Mzungu

Dejan Mzungu Zoran humwambii kitu kwa Mzungu

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA wa Simba, Zoran Maki, amesema kuwa mashabiki wa timu hiyo wasiwe na haraka na uwezo wa mshambuliaji wa timu hiyo, Dejan Georgejevic, kwani tayari ameshaanza kuwaonyesha ubora wake wa kufunga ndani ya timu hiyo.

Dejan ambaye ni ingizo jipya, tayari amefanikiwa kufungua akaunti ya mabao ndani ya Simba mara baada ya kufunga bao katika mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ambapo Simba walicheza dhidi ya Kagera Sugar.

Kocha Maki alisema kuwa kwa wale wote ambao walikuwa wanahoji ubora na uwezo wa Dejan wanatakiwa kutulia kwani tayari wamejionea uwezo wake na ni jambo la subira kwa mchezaji mpya katika timu yoyote kuanza kwa kufanya vizuri.

“Wanatakiwa kuangalia kuifutilia timu kwa ukaribu lakini kuhusu Dejan labda huko mbeleni ndio walitakiwa kuhoji kuhusu ubora wake na sio kwa sasa kwani ni mapema mno kwa mchezaji mpya ndani ya timu.

“Lakini pia watakuwa wamejionea uwezo wake wa kufunga kupitia mchezo dhidi ya Kagera, kila kitu kitakuwa sawa, sio pekee tu kuna wachezaji wengine wengi tunaamini watakuja kutusaidia sana huko mbeleni na sio mapema hii na huo ndio mpira,” alisema kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live