Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto Kabwe ataka Serikali iruhusu uraia pacha

Zitto Kabwe Drt Zitto Kabwe ataka Serikali iruhusu uraia pacha

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia taarifa za mchezaji Benard Kamungo kujumuishwa kwenye kikosi cha Olimpiki cha Timu ya Taifa ya Marekani na kuzua gumzo kwenye mitandao mbalimbali, Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amechapisha maneno haya kwenye mitandao yake ya kijamii:

"Serikali ya Tanzania ifanye maboresho ya Sheria ya Uraia ili kuruhusu Watu wenye nasaba na Tanzania kuwa na Uraia pacha.

"Chama chetu cha ACT Wazalendo kinatoa msisitizo kwamba tunapoelekea ku-host mashindano ya AFCON 2027 na matayarisho ya Kombe la Dunia 2026, turuhusu kisheria Vijana wetu wenye vipaji kuwa na passport zaidi ya moja. Kuzuia uraia pacha kunatugharimu kama nchi."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live