Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zinchenko arudi kundini Arsenal

Zichenko Zinchenko arudi kundini Arsenal

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: Dar24

Kikosi cha Arsenal kimepata mzuka zaidi kwenye vita yao ya kusaka ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu baada ya kurejea mazoezini kwa staa wao Oleksandr Zinchenko.

Beki huyo wa kushoto alikosa mechi ya sare ya 2-2 dhidi ya West Ham United mwishoni mwa juma lililopita kutokana na kuwa majeruhi ambapo alichezeshwa Kieran Tierney.

Hata hivyo mkali huyo anaonekana kuwa amepona maumivu yake ya misuli aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Liverpool majuma mawili yaliyopita.

Zinchenko anatazamiwa kuwa fiti kwa ajili ya mechi ya Southampton itakayopigwa badae leo Ijumaa (April 21).

Baada ya mchezo huo dhidi ya Saints, chama hilo la Mikel Arteta litajiandaa na mchezo mgumu na muhimu zaidi kwenye mbio za ubingwa wa ligi wakati itakapokwenda kuwakabili Manchester City uwanjani Etihad, Jumatano ya Juma Lijalo.

Arsenal kwa sasa inashika usukani wa ligi kwa tofauti ya alama nne dhidi ya Man City ya Pep Guardiola, ambao wana mchezo mmoja mkononi.

Chanzo: Dar24