Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zinchenko arejea Mazoezini Arsenal

Zinch Return Zinchenko arejea Mazoezini Arsenal

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinzi wa kushoto wa klab ya Oleksandr Zinchenko (26) amereja rasmi mazoezini baada ya kupona majeraha yake,

Sasa Zinchenko ametuliza presha kwenye kambi ya Arsenal baada ya kurejea uwanjani na atakuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho Jumatatu dhidi ya Crystal Palace utakaopigwa Selhurst Park.

Beki huyo wa kushoto kutoka Ukraine alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya kigimbi tangu mwishoni mwa msimu uliopita, lakini siku mbili zilizopita alirejea mazoezini na kufanya vizuri.

Zinchenko sasa atampa Kocha Mikel Arteta uhakika wa kumtumia kwenye nafasi hiyo baada ya miamba hiyo ya Emirates kumpoteza staa wake mpya, Jurrien Timber, aliyeumia goti kwenye mechi ya kwanza ya ligi msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live