Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zimevuja! Anayetaka kumng'oa Lomalisa Yanga ajulikana

Bangala X Lomalisa Bangala na Lomalisa

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zmevuja! Ndiyo utakavyoweza kusema ni baada ya sababu kujulikana za beki wa kushoto wa Yanga, Mkongomani Joyce Lomalisa Mutambala kuomba kuvunja mkataba.

Beki huyo mwenye uwezo mkubwa wakupiga krosi, wiki iliyopita ilielezwa kuandika barua ya kuomba mkataba wake wa mwaka ambao ameubakisha hapo uvunjwe.

Hiyo ikiwa siku chache zimebakia kabla ya usajili mkubwa wa msimu ujao kufunguliwa, ili timu shiriki za Ligi Kuu Bara zianze kufanya usajili wake.

Mmoja wa Mabosi wa Benchi la Ufundi la timu hiyo, amesema, sababu kubwa ya beki huyo kuomba kuvunja mkataba ni kutofurahia kuwekwa benchi na kiraka Kibwana Shomari anayemudu kucheza nafasi zote za beki wa pembeni.

Bosi huyo alisema kuwa Lomalisa anataka kuondoka hapo ili aende kwingine akapate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, lakini sio kuendelea kubakia hapo awekwe benchi na Kibwana.

Aliongeza kuwa uongozi umekubali kumuachia beki huyo aondoke, lakini kwa sharti la kuiita mezani klabu anayotaka kwenda kwa ajili ya kufanya mazungumzo rasmi.

“Uongozi tayari umemwambia kuwa upo tayari kumuachia aondoke hapo, lakini hiyo timu inayomtaka ije kwa uongozi wa Yanga kwa ajili ya mazungumzo.

“Kwani sababu yake inayomfanya avunje mkataba ya kitoto, kikubwa yeye kama anataka kucheza katika kikosi cha kwanza aongeze bidii ya kupambana uwanjani kila atakapopata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: