Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zile fedha za ujenzi wa uwanja Bunju ishu iko hivi

Mo Arena Bunju Simba Bunju

Sun, 21 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba imetoa majibu juu ya sintofahamu ya michango ya fedha  za ujenzi wa uwanja wao wa MO Simba Arena.

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amesema jumla ya Sh275 milioni zilichangwa na wanachama na mashabiki wao kwa ajili ya ujenzi huo.

Mangungu amesema mbali na michango hiyo pia kulifanyika mchakato wa 'nani ni nani' uliosimamiwa na Azam Tv na fedha hizo zimetumika kwenye ujenzi na maboresho yaliyokusudiwa.

"Fedha hizo zote zimetumika kujenga uzio wa eneo letu la Bunju kwa wanaoweza kufika kule waende wataona jinsi kazi iliyofanyika.

"Tumeboresha pia hosteli zetu pale Bunju zimekuwa za viwango vya juu ambazo sasa timu yetu inazitumia inapokuwa mazoezini.

"Bado kazi inaendelea ya kufanya maboresho, tumeona tutoe mrejesho huu ili watu wajue na kuacha upotoshaji juu ya hizi fedha."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live