Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zawadi Mauya kutua Singida Black Stars

Mauya 2 Zawadi Mauya

Sun, 30 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa kiungo mkabaji wa Yanga, Zawadi Mauya akimaliza rasmi mkataba katika klabu ya Yanga SC, Klabu ya Singida Black Stars iko kwenye hatua za mwisho za kumsajili.

Kiungo huyo mkabaji alisajiliwa na klabu ya Yanga July 2020 akitokea katika klabu ya Kagera sugar FC. Kwa wachezaji waliopo kwa sasa yeye ndiye mchezaji aliyedumu kwa muda mrefu katika kikosi cha Yanga.

"Yanga ni klabu iliyo na mipango mikubwa. Kama mchezaji nilijifunza kuendana nayo, nimepata ujuzi kutoka kwa makocha tofauti"

"Kitendo cha kucheza wazawa na wageni kimeniongezea mambo mengi katika majukumu yangu. Kikubwa naamini ninachokifanya sio wanachokiona wengine kwangu" - Zawadi Mauya.

"Zipo alama nyingi za kumbukumbu nzuri kutoka katika klabu ya Yanga, siwezi kutaja moja baada ya nyingine ingawa kwa msimu uliopita sikuwa na nafasi kubwa ya kucheza, hivyo haukuwa mzuri kwangu kiwanjani ila ulikuwa bora kwa klabu yangu kunyakua mataji yote muhimu.

"Ndoto zangu za kuvaa medali za Ubingwa zimetimia nikiwa Yanga SC," amesema Zawadi Mauya

Chanzo: www.tanzaniaweb.live