Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar yaomba kuandaa Cecafa 2024

Cecafa Picff Zanzibar yaomba kuandaa Cecafa 2024

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF), limethibitisha kukamilisha maombi ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya CECAFA Senior Challenge 2024, yanayotarajiwa kufanyika Julai, mwaka huu.

Mataifa washindi wa tenda hizo wanatarajiwa kutangazwa katika Mkutano Mkuu wa wa Cecafa utakaoafanyika Februari 23, 2025 jijini Mombasa, Kenya.

ZFF imefanya hivyo baada ya Cecafa kutangaza nafasi za kuwania kuandaa mashindano mengine matano yatakayofanyika mwaka 2024 ambayo ni;

Kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika 'Afcon' kwa wanaume chini ya miaka 17 na 20, (AFCON U-17 Boys qualifiers), na (AFCON U-20 Boys qualifiers), kuwania kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake ngazi ya klabu (CAF Women’s Champions League Zonal qualifiers), kuwania kushiriki michuano ya kutafuta Bingwa wa Shule za Afrika (Africa Schools Football Championships Zonal qualifiers), pamoja michuano ya Ubingwa wa CECAFA kwa Wanawake chini ya umri wa miaka 20 (CECAFA U-20 Girls Championship).

Cecafa Senior Challenge ni miongoni mwa michuano ya muda mrefu zaidi Afrika yanayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika na Kati (CECAFA), yakiwa yameanzishwa mwaka 1926 yakijulikana kama Gossage Cup na mechi ya kwanza ilipigwa mwaka huo kati ya Uganda na Kenya iliyoshinda mabao 2-1.

Mashindano hayo yanayoshirikisha nchi wanachama wa baraza hilo na yanatambulika na Shirikisho la Soka duniani (Fifa), ni Tanzania, Uganda, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Burundi, Somalia, Rwanda, Sudan na Kenya.

Mara ya mwisho kwa michuano hiyo kufanyika ni Desemba mwaka 2019, Uganda na wenyeji kutwaa ubingwa huo baada ya kuichapa Eritrea mabao 3-0 kwenye mechi ya fainali iliyopigwa dimba la Lugogo, jijini Kampala.

Wakati huo timu shiriki zilikuwa tisa, Uganda, Burundi, Djibouti, Eritrea, Kenya, Somalia, Sudan, Tanzania na Zanzibar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live