Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar na vipaji vya mashuti

Shekhan Zanzibar na vipaji vya mashuti

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Visiwa vya Zanzibar ni moja ya sehemu iliyobarikiwa kuzalisha viungo wazuri ambao wamekuwa na msaada mkubwa sana kwenye soka la Tanzania miongoni mwa viungo hao wanaotoka visiwani Zanzibar wapo ambao wamejaaliwa na Mwenyezi Mungu uwezo wa kupiga mashuti ya mbali halafu makali yaani mazito.

Miongoni mwa viungo hao wenye mashuti makali kutoka visiwani Zanzibar ni Abdi Kassim Babi huyu kutokana na uwezo wake wa kupiga mashuti ilepelekea mchambuzi maarufu hapa Tanzania Edo Kumwembe kumbatiza jina la Ballack wa Unguja.

Ikumbukwe Babi ndie mchezaji wa kwanza kufunga goli Uwanja wa Mkapa mechi ya kirafiki dhidi ya Uganda alifunga goli ambalo ni shut la masafa marefu na kali na mwixho wa game Tanzania ilibuka mshindi kwa 1-0.

Feisal Salum Abdallah, nae ni moja ya viungo hatari kwa soka la Tanzania nae ni moja ya viungo kutoka Zanzibar ambae amejaaliwa kuwa na uwezo wa kupiga mashuti makali na ya mbali yenye uzito mkubwa pia ikumbukwe kuwa Feisal kwenye magoli yale yote assilimia 78 ni ya mashuti makali.

Mudathir yahya Abbas moja ya viungo watulivu wakiwa uwanjani nae sometime hupiga mashuti japo sio mara nyingi kama wengine.

Wengine ni kama Almarhum Ibrahim rajab Jeba, Abdulswamak Kassim, Abdulhalim, Khamis Mcha Vial, Mo banka, Abdul Aziz Makame na wengineo kwa vizazi tofauti.

Kwasasa kuna kiungo pale kwa Wananchi anaitwa Shekan Ibrahim Khamis ni ongezeko jingine la viungo wa Kizanzibar wenye mashuti makali na mazito anatumia guu la kushoto mara nyingi kwenye kupiga (shot) ni moja ya wachezaji vijana wenye uwezo mzuri sana kwenye kupiga mashuti mpk sasa magoli aliyofunga akiwa na JKU FC, Zanzibar Hereous U18 na sasa Yanga assilimia 67 ya magoli yake ni makombora.

Kama uliangalia mechi ya ya Yanga dhidi ya APR licha ya Yanga kupoteza game kwa 3-1, Shekan Ibrahim aliingia kwa kutokea sub na dakika chache alizocheza alionesha uwezo wake wa kushuti kwa kupiga makombora 3, mawili yalilenga lango na moja halikulenga lango. Mimi ninambatiza Shekhan kwa jina la The Shoter.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live