Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar kuandaa CECAFA 2024

Yeyeye 1000x600 Zanzibar kuandaa CECAFA 2024

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup inatarajia kufanyika visiwani Zanzibar kuanzia Juni 29 hadi Julai 14, 2024.

Mwezi uliopita Zanzibar ilithibitisha kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa ya CECAFA kupitia Mkutano Mkuu uliofanyika Mombasa, Kenya.

“Baada ya mazungumzo na wadhamini wetu Azam TV, tumeamua kuwa, Juni 29 hadi Julai 14 utakuwa wakati mzuri kufanyika kwa mashindano ya CECAFA Senior Challenge Cup,” amesema Auka Gecheo.

Ametoa wito kwa wanachama wa CECAFA ambao timu zao zitashiriki, kuchangia kiasi cha dola za Marekani 20,000 ambazo zitatumiwa na mwenyeji wa mashindano kwa ajili ya kutoa huduma.

Gacheo amesema kuna uwezekano wa kualika timu kutoka kwenye Kanda nyingine ili kuleta mvuto na ushindani kwenye mashindano ambayo pia yatasaidia timu za taifa za ukanda wa CECAFA kujiandaa kuelekea mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 na AFCON 2025.

Michuano ya CECAFA Challenge Cup itarejea baada ya kufanyika mara ya mwisho miaka minne iliyopita [2019]. Wenyeji Uganda waliifunga Eritrea kwenye mchezo wa Fainali.

Mbali na CECAFA Senior Cup, mwaka huu kutakuwa na mashindano mengine matano.

CAF Women’s Champions Lague Zonal qualifiers [Ethiopia]

AFCON U-20 Boys Zonal qualifiers [Tanania]

African Schools Football Championship Zonal qualifiers [Zanzibar]

CECAFA U-20 Women’s. Championship [Ethiopia]

AFCON U-17 Boys qualifiers [Uganda].

Chanzo: www.tanzaniaweb.live