Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zanzibar Heroes, Kilimanjaro Stars acha tuone

Mastaa Stars KK Zanzibar Heroes, Kilimanjaro Stars acha tuone

Wed, 27 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uwanja wa Amaan, mjini Unguja uliokarabatiwa na kuwa na mwonekano wa kisasa, unatarajiwa kuzinduliwa leo ukisindikizwa na burudani mbalimbali ikiwamo ya muziki mapema, lakini kuanzia saa 2:15 usiku litapigwa bonge la mechi la wanandugu, Zanzibar Heroes na Kilimanjaro Stars ya Tanzania Bara.

Mechi hiyo maalumu imekuwa gumzo kwa mashabiki visiwani hapa kutokana na ushindani unaojitokeza kila timu hizi zinapokutana, ingawa safari hii unatumika pia kumrahisishia kazi Kocha Mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars kusaka kikosi cha kwenda nacho Fainali za Kombe la Afrika Afcon.

Michuano hiyo inafanyikia Ivory Coast kuanzia Januari 13-Februari 12 mwakani, huku Kocha Adel Amrouche akiwa ameita kikosi cha wachezaji 53 wakiwamo wanaounda timu hizo mbili zinazoumana leo.

Tayari Stars imeshatinga visiwani hapa na kocha Mualgeria Adel, huku Zanzibar Heroes ikinolewa na msaidizi wa kocha huyo, Suleiman Hemed ‘Morocco’ na kwa siku mbili amekuwa akiwapa madini na mbinu vijana wa timu hiyo ili kujiandaa na pambano hilo.

Utamu wa mechi hiyo ni rekodi zilizopo baina ya timu hizo, mara nyingi huwa pambano linakuwa na ushindani mkubwa na rekodi zinaonyesha tangu mwaka 1964 katika mechi tofauti ilizokutana zikiwamo za michuano ya Kombe la Chalenji, Bara imeshinda 13 na Zanzibar ikishindia saba na mbili ziliisha kwa sare.

Mbali na burudani ya soka kutoka kwa nyota wa timu hizo, bara ikiwa na majembe 25 na Zenji ikiita 29, lakini mapema wasanii mbalimbali akiwamo Khadija Kopa na wengine watatumbuiza na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi atakayezindua uwanja huo wa Amaan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live