Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zambia wana watu

Paston Daka Kalaba Zambia wana watu

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rainford Kalaba ni Moja ya majina ambayo yalitamba kwenye Soka la Afrika, nyota huyu Raia wa Zambia alifanya makubwa AFCON 2010 pale Angola na AFCON 2012 pale Gabon.

Kalaba akicheza kama kiungo mshambuliaji alikuwa bora sana kwenye kutengeneza nafasi za kufunga ndiyo maana Kinda Emmanuel Mayuka alitamba AFCON 2012 Hadi kuwa Moja ya vinara wa kuchana nyavu katika michuano hii wakati Zambia inatwaa Taji.

Nahodha wa Zambia nae Christopher Katongo alitangazwa kuwa mchezaji bora, huyu alitengeneza pacha Moja ya hatari sana na Rainford Kalaba bila kusahau Emmanuel Mayuka ambaye alikuwa anaingia kutoka benchi kuchukua nafasi ya James Chamanga .

Miaka imekwenda Kasi sana leo Zambia wanaenda AFCON wakiwa na nyota wao Patson Daka ambaye wanaamini atawaongoza kufanya makubwa katika michuano hii.

Kizazi cha Kalabu na wenzake watabaki kuwa Mashujaa pale Zambia Kwa muda mrefu kwa sababu nyota wao wengi walikuwa TP Mazembe na Ligi Kuu ya Afrika Kusini lakini waliiongoza Zambia kuwa Bingwa wa Mataifa ya Afrika mbele ya vigogo kama Ivory Coast ambao wachezaji wao wote walikuwa wanacheza Ligi kubwa za Ulaya zile Top 5.

Inawezekana Zambia ya leo ina wachezaji wengi wanaocheza nje ya Afrika kuliko Zambia ya 2012 ila ile ilikuwa na Kikosi ambacho kilikuwa na uchungu mkubwa na Taifa lao Kila mchezaji alijitoa Kwa moyo wake wote kuipa mafanikio timu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live