Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zambia, Morocco wafuzu nusu fainali WAFCON 2022

WAFCON PIC.jpeg Wenyeji wa michuano ya WAFCON 2022 Timu ya taifa ya wanawake ya Morocco

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: eatv.tv

Timu ya taifa ya Zambia ya Wanawake imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya AFCON ya Wanawake baada ya ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Senegal kufuatia sare ya bao 1-1 kwenye mivhezo ya kwanza ya mtoano iliyoanza usiku wa Julai 13, 2022.

Senegal walikuwa wa kwanza kupata goli katika dakaika ya 61 liliofungwa na Nguenar Ndiaye, kisha Zambia wakasawazisha dakika ya 70 kupitia kwa Avell Chitundu.

Na mchezo wa pili uliwakutanisha wenyeji wa michauno hiyo Morocco dhidi ya Botswana ambapo wenyeji waliibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja.

Morocco ndio walikua wakwanza kupata goli la mapema katika dakika ya tatu tu ya mchezo kupitia kwa Sanaa Mssoudy kisha Keitumetse Dithebe akawazasazishia Botswana katika dadika ya saba, na baadae Yasmin Mrabet akawaweka kambani goli la ushindi kwa wenyeji dakika 59 kipindi cha pili.

Baada ya Zambia na Morocco kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa ya soka la wanawake barani Africa, leo Alhamis July 14 michuano hiyo itaendelea tena kwa michezo miwili ya robo fainali iliyobaki ambapo Cameroon wataumana na Nigeria majira ya saa 2:00 usiku, huku Afrika Kusini wakikutana na Tunisia majira ya saa 5:00 usiku.

Chanzo: eatv.tv