Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zamalek yapigwa nyundo Misri kisa Al Ahly

Ahly Zamalek Zamalek yapigwa nyundo Misri kisa Al Ahly

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha soka nchini Misri kimeipa adhabu klabu ya Zamalek SC kwa kosa kuficha mipira wakati mchezo wa Cairo derby Zamalek dhidi ya Al Ahly SC.

Klabu ya Ahly wamepeleka malalamiko hayo kuhusu ucheleweshaji wa kurudisha mipira eneo la kuchezea.

Kwa tuhuma hizo klabu ya Zamalek imepewa adhabu pamoja na kutozwa faini ya EGP 50,000 sawa na kiasi cha shilingi milioni 2.6 za Kitanzania, huku viongozi ndani ya benchi la ufundi kusimamishwa michezo 2, mwingine amesimamishwa kwa michezo 4.

Mchezo huo ulipigwa juzi Aprili 15, 2024 na Zamalek wakiwa nyumbani kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dakika ya 44 na 86.

Mabao yote ya Zamalek yalifungwa na Seifeddine Jaziri huku bao la Ahly likifungwa na Ahmed Mohamed Abdel Kader Radwan dakika ya 73.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live