Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zamalek yaondoshwa Ligi ya Mabingwa, Belouizdad yatinga Robo Fainali

Zamalek Belouizdad .jpeg Zamalek yaondoshwa Ligi ya Mabingwa, Belouizdad yatinga Robo Fainali

Sat, 18 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miamba ya soka ya Misri, Zamalek imeaga michuano ya klabu Bingwa Afrika kufuatia kichapo cha pili dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria.

Belouizdad imetinga hatua ya robo fainali na inaungana na Esperance ya Tunisia, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Raja Casablanca ya Morocco kwenye 8 bora.

Mchezo wa Zamalek umepigwa nyumbani kwao, katika Dimba la Nelson Mandela, Baraki nchini Misri.

FT: CR BELOUIZDAD 2-0 ZAMALEK SC

⚽ Zakaria Draoui (75')

⚽ Leonel Wamba (79)

FT: Al Merreikh 1 - 1 Esperance de Tunis

⚽ M. Hammouda (23)

⚽ Paulo Sérgio (90 pen)

MSIMAMO KUNDI D

1. ES Tunis — 10 ✅

2. CR Belouizdad — 9✅

3. Al Merreikh — 5 ❌

4. Zamalek — 4❌

Inelezwa kuwa, mashabiki wa Zamalek waliwazomea sana wapinzania wao, Al Ahly kufuatia kipigo cha 5-2 dhidi ya Mamelodi Sundowns, jana Zamalek imeaga huku Al Ahly ikiwa na matumaini japo kidogo ya kusonga mbele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live