Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zamalek yagomea mechi na Al Ahly

Ahly Zamalek Ms Zamalek yagomea mechi na Al Ahly

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha vilabu vya soka nchini Misri kimetangaza rasmi kuahirisha mechi ya wahasimu wa jadi nchini humo, Al-Ahly dhidi ya Zamalek katika mechi ya raundi ya 27 ya ligi hiyo.

Red Giant ilitarajiwa kukutana na White Knight katika Raundi ya 27 ya Ligi Kuu nchini humo leo Jumanne, Juni 25, 2024 lakini Zamalek iligoma na kusema kwamba haitacheza mechi hiyo.

Bodi ya Ligi ilitoa taarifa rasmi kwamba kulingana na barua ya Klabu ya Zamalek kwa Ligi kuhusu kuomba Al-Ahly amalize vipori vyake kwanza na timu zote zilingane mechi ndipo wakutane.

Zamalek ilitangaza kuwa haitacheza mechi yoyote baada ya kumaliza mechi ya Pharco kabla ya timu zingine kucheza mechi sawa za mzunguko wa ligi.

Katika msimu wa Ligi, ambapo Pyramids wanaongoza wakiwa na alama 62 katika michezo 25, Al Ahly wapo nafasi ya pili na alama 42 katika michezo 18 wakati Zamalek wakiwa nafasi ya 10 na alama 34 kwenye michezo 20.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live