Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zamalek waibuka mabingwa wa Kombe la Shirikisho CAF

Zamalek Msd Zamalek waibuka mabingwa wa Kombe la Shirikisho CAF

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Zamalek imepindua meza baada ya kupoteza mechi ya mkondo wa kwanza na kushinda ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CAF.

Alikuwa ni mshambuliaji Ahmed Hamdi aliyethibitisha ushindi wa Zamalek, na kuifungia Zamalek bao pekee kwenye mchezo huo dakika 23 na kusawazisha kwa jumla ya mabao (Aggregate 2-2).

Zamalek ilipoteza katika mechi ya kwanza kwa bao 2-1 nchini Morocco na kufanikiwa kupindua meza kwenye mchezo wa marudiano katika Uwanja wa Kimataifa wa Cairo na kuwafanya Zamalek kutwaa ubingwa huo kwa mara ya pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live