Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zamalek waanza na Kichapo Ligi ya Mabingwa

Zamalek FC Lost Mchezo ulimalizika kwa Zamalek kukubali kichapo cha bao 1-0

Sat, 11 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika timu ambayo nayo imeanza vibaya kwenye michuano ya kabu bingwa ni pamoja na Zamalek ambaye amechapwa bao 1-0 akiwa nyumbani kwake dhidi ya CR Belouizdad ya huko Algeria.

Bao hilo lilipachikwa kwenye kipindi cha pili cha mchezo huku bao hilo likifungwa kwa mkwaju wa penati na kuifanya timu hiyo kujivunia pointi tatu katika kundi hilo D huku mwenyeji akiwa haamini yanayotokea.

Zamalek kwenye ligi msimu huu hayupo vizuri baada ya klushikilia nafasi ya sita kwenye msimamo baada ya kucheza mechi zake 17 na kijipatia pointi 29 huku wapinzani wao wakubwa Al Ahly wakiwa ndio vinara wa ligi hiyo.

Timu hiyo imeachwa pointi 8 na kinara wa ligi huku ikiwa tayri imepoteza michezo minne kwenye ligi na matumaini ya kushindania taji la ligi hiyo yakiwa ni hafifu kabisa.

Baada ya kupoteza mchezo huo, timu hiyo itarejea kwenye ligi kumenyana dhidi ya Smouha, kabla ya kukiwasha dhidi ya Al Merreikh 17 Februari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live