Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zamalek kutua Azam Complex wiki hii

Zamalek FC Kikosi cha Zamalek

Wed, 5 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa Ligi Kuu mara 20 ya nchini Misri Zamalek FC wanatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam wiki hii kwa ajili ya kuikabili klabu ya Flambeau du Centre ya Burundi katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumamosi kwenye uwanja wa Azam Complex huku wenyeji wa mchezo huo Flambeau du Centre nao wanatarijiwa kutua nchini siku za hivi karibuni.

Awali klabu hizo zilifikia makubaliano ya kucheza mechi zao zote mbili nchini Misri.

Hata hivyo mabingwa hao wa Burundi hautakuwa mchezo wao wa kwanza kwenye Uwanja wa Azam Complex kwani mechi yao dhidi ya Al Attihad ya Libya walicheza kwenye uwanja huo ambapo waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live