Zama za Obrey Chirwa ndani ya Azam FC walipokutana na Simba ilikuwa kazi kubwa kumzuia kwa mabeki wakiogozwa na Joash Onyango.
Mechi zao zote wanapokutana uwanjani huwa sio nyepesi na kwenye ligi msimu huu Azam FC wamesepa na pointi nne huku Simba wakisepa na pointi moja.
Kwa sasa Chirwa yupo zake ndani ya Ihefu akipambania ugali wake huku Onyango akiwa bado yupo ndani ya Simba.
Miongoni mwa mabeki wenye uwezo mkubwa ndani ya Simba akianza kutimiza majukumu yake na amekuwa akifanya makosa yanayoigharimu timu pale anapokuwa hayupo sawa.
Ikumbukwe kwamba ni chaguo la kwanza Onyango la Roberto Oliveira kwa sababu hakuna beki mwingine ambaye anaweza kumpa changamoto kwenye kugombea naye namba.
Kituo kinachofuata ni Mei 7, Azam FC v Simba mchezo wa hatua ya nusu fainali Kombe la Azam Sports Federation, Uwanja wa Nangwanda Sijaona.