Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zama mpya Madrid majira ya Kiangazi

Super League Perez Modric Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amepanga kufanya sajili kubwa dirisha lijalo

Mon, 29 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Carlo Ancelotti amedai kuwa Rais wa Real Madrid Florentino Perez anajipanga kuleta maboresho katika timu ya Real Madrid hasa katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Kocha huyo wa Kiitaliano alibaini kuwa malengo ya Los Blancos yapo sawa, licha ya changamoto za kifedha katika kandanda uliosababishwa na janga la COVID-19.

“Real Madrid, kila kitu ni sawa na hakijabadilika,” Ancelotti aliambia Corriere dello Sport.

“Kitu pekee kinachobadilika ni makocha tu. Nguvu ileile, wafanyakazi wale wale, waandishi wa habari wale wale, maono sawa, uharaka sawa, licha ya changamoto za kiuchumi uliosababishwa na janga hili.

“Katika mwaka mmoja, mwishoni mwa Desemba 2022, Estadio Santiago Bernabeu mpya itakuwa tayari na Florentino ana mipango mikubwa ya Julai.

“Florentino ana nia nzuri sana Kumsaini Erling Haaland pamoja na Kylian Mbappe Hebu tuzungumze kuhusu hilo baadaye”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live