Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zakazakazi ataka bao la Kipre lichukue "PUSKAS"

Kipre X Zaka Zakazakazi ataka bao la Kipre lichukua "PUSKAS"

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la soka duniani, FIFA, hutoa tuzo ya bao bora la mwaka, ambayo huitwa tuzo ya Puskas.

Iliitwa hivyo kwa heshima ya Ferenc Puskas, nyota wa zamani wa Real Madrid ya Hispania na timu ya taifa ya Hungary.

Mwamba huyu anachukuliwa kama supastaa wa kwanza wa kimataifa wa mpira wa miguu.

Aliichezea timu yake ya taifa katika mechi 85 na kufunga mabao 84.

Katika maisha yake ya soka alicheza mechi 793 na kufunga mabao 806.

Kutokana na sifa zake za kufunga, FIFA ikamuenzi kwa kuanzisha tuzo hizo.

Ili bao liwe na sifa ya kuwania tuzo hii lazima liangaliwe kwa vigezo vifuatavyo.

1. Move

2. Technique

3. Skills

Nitachambua kigezo kimoja kimoja kama ambavyo FIFA wamevutaja

1. MOVE

Ni namna shambulizi lililozaa bao lilivyojengwa; iwe kitimu au kwa juhudi binafsi.

i. Bao linaweza kufungwa baada ya pasi nyingi au timu zima kupasiana bila wapinzani kugusa mpira.

ii. Bao linaweza kufungwa kwa mchezaji mmoja kuwapiga chenga wapinzani kadhaa au wote.

2. TECHNIQUE

Ni maarifa ya mchezaji anapokuwa na mpira bila kumhusisha mpinzani.

Kwa mfano kupiga shuti, kuupokea mpira (kuua) kwa kifua, kisigino au vyovyote vile.

Mabao ya tiktak, mashuti ya mbali, vichwa vya mbizi au rabona huangukia hapa.

3. SKILLS

Ni maarifa ya mchezaji anapokuwa na mpira na mpinzani. Hapa ndipo kuna chenga (vyenga), kanzu, matobo, kupimana a umri, nk.

BAO LA KIPRE

Kwenye bao hili la Kipre, sifa zote hizi unazikita.

Move -Kipre alifunga bao hili kwa move ya juhudi binafsi, akikimbia na mpira karibu robo tatu ya uwanja.

Skills

Kipre aliwapiga chenga wachezaji wengi wa timu pinzani huku akiwapima umri. Pia kitendo chake cha kwenda na mpira pembeni ya uwanja kikamdanganya kipa na kudhani atapiga krosi.

Haya yote ni maarifa ambayo Kipre aliyaweka kwenye bao hili na kumuongezea sifa.

Technique

-Kipre alimalizia shambulizi lake kwa kufunga kwa technique ya hali ya juu. Alimchungulia kipa na kuona ametoka kidogo, akamuinulia kwa juu...waya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live