Nilikuwa nasubiri kwa hamu kubwa sana kuona kipindi cha kipyenga cha mwisho kitakavyochambua matukio tata ya mchezo wa Dar Es Salaam Derby kati ya Azam FC na Yanga.
Lakini nasikitika kusema kipindi kimeniangusha sana. Uchambuzi wake haukufanywa katika hali ya kukata kiu cha mtu aliyetaka kuona HAKI.
Nasikitika kusema waamuzi wa mchezo ule walikuwa bora kuliko kipindi.
Pata picha kipindi kilipata faida ya kurudia video ya mchezo kwa siku nne, lakini bado hakikutenda haki kuliko waamuzi.
BAO LA PILI LA AZAM FC
Hisia za wengi zilikuwa kwenye bao la pili la Azam FC. Wengi tulisubiri kuona utata utakavyotatuliwa, badala yake utata ndiyo umekuwa mkubwa ziadi.
Mchoro uliotumika una shida zaidi. Mstari hutakiwa kuchorwa kuanzia pale mpira unapotoka kwa mpigaji wa pası ya mwisho.
Lakini kwenye kipindi mchoro uliwekwa kabla mguu wa mpigaji haujafika kwenye mpira.
Hapa kawahi kuuchora kabla ya tukio lenyewe…hadi mguu wa mpigaji ufike kwenye mpira, SECOND LAST DEFENDER wa Yanga tayari alishasogea mbele na kuua OFFSIDE.
ZAIDI YA HAPO
Kuna matukio mengine mengi ambayo tulitarajia kuona yakichambuliwa lakini haikuwa hivyo.
OFFSIDE YA KIPRE
Kipre Jr wa Azam FC alihukumiwa kuotea kwenye tukio la wazi kuliko hata la Gibril Sillah.
Hii ilikuwa nafasi ya wazi kwa Azam FC kupata bao kuliko ya Sillah, lakini Kipyenga hakikuona umuhimu.
SOPU VS YAO YAO Dakika ya 31, Abdul Sopu alifanyiwa madhambi na Yao Yao. Mwamuzi hakuhukumu na kipyenga hakikujadili kabisa.
FEI VS MUDATHIR Dakika ya 8, Mudathir Yahya alimfanyia madhambi Feisal Salum na mwamuzi hakuhukumu…kipyenga hakikujadili.
KIPRE VS LOMALISA Dakika ya 73, Lomalisa alimuangusha Kipre, mwamuzi hakuhukumu na kipyenga kikakaa kimya.
FEI VS GUEDE Dakika ya 76, Guede alimsukuma Feitoto, mwamuzi msaidizi akahukumu kwamba madhambi yaelekee Azam (ajabu), lakini mwamuzi wa kati akaacha mpira uendelee…ajabu zaidi ni kwamba kipyenga nacho hakikuona.
ADOLF VS SURE Dakika ya 13, Sure Boy alimfanyia madhambi Adolf Mutasingwa, mwamuzi hakuhukumu na kipyenga kikakaa kimya.
BACCA VS MSINDO Dakika ya 15, Bacca alifanya tacking mbaya na kumuumiza Msindo…mwamuzi hakuhukumu na kipyenga kikakaa kimya.