Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zakazakazi amvaa Jemedar Said kisa Kocha Dabo

Zakazakazi Hj.jpeg Thabit Zakaria "Zakazakazi" - Afisa Habari wa klabu ya Azam FC

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa habari wa Azam Fc Thabit Zakaria "Zaka za Kazi" amemjia juu mchambuzi wa vipindi vya michezo kwenye radio, Jemedari Said (Bin Kazumari) kuhusu taarifa anazochapisha kwenye mtandao wake wa kijamii kuhusu kocha wa Azam Fc Youssuf Dabo raia wa Senegal

Anaandika Zaka Zakazi;

Mchambuzi nguli Jemedari Said amerudia tena kuandika taarifa potoshi kuhusu kocha Yousouph Dabo wa Azam FC.

Nasema amerudia tena kwa sababu mara ya kwanza ilikuwa Agosti 13 kwenye ngao ya jamii, alipoandika kwamba Dabo ana Leseni B ya CAF ambayo imeshapitwa na wakati.

Na akashangaa kwanini TFF inamuacha anakaa kwenye benchi.

Baada ya pale ligi ikaanza na Dabo akakaa kwenye benchi...na zikafuata mechi za CAF, akakaa tena kwenye benchi.

Najua Jemedari alimuona Dabo kwenye benchi, ila sijui kama aliendelea kushangaa.

Safari hii karudia tena kuandika kuhusu Dabo, akisema 'tuliaminishwa kwamba ana Pro License.'..mliaminishwa na nani bwana Jemedari?

Wewe ndiyo uliaminisha watu kwamba Dabo ana Leseni B ya CAF iliyopitwa na wakati....na hakuna aliyekujibu, siyo Azam FC wala TFF uliowashangaa.

Sasa unakuja na hoja nyingine...kwanini lakini meneja wetu wa zamani? Wewe si una access na Azam FC na hata TFF, kwanini usiwaulize ili kubalansi stori?

Ni hivi, wale TFF uliowashangaa, walimuacha Dabo kwenye benchi kwa sababu ana Leseni A ya UEFA.

Hii inamfanya atoshe kukaa kwenye benchi bila shida.

Na ameipatia Ufaransa katika kituo cha ufundi cha shirikisho la soka la Ufaransa, Claire fontaine.

Yaani kama ni chuo kikuu, basi hiki ndiyo chuo kikuu namba moja cha soka Ufaransa.

Kwa sheria na kanuni za Tanzania ambazo zilianzia CAF, ni kwamba kocha mwenye Leseni A ya UEFA akija huku anahesabika sawa na Leseni B.

Na Leseni B haitoshi kuwa kocha mkuu bali msaidizi...ndiyo maana Dabo ameorodheshwa kama kocha msaidizi.

Dabo ana Leseni A ya UEFA!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live