Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zakazakazi amlipua Oscar Oscar, ampa somo zito

Oscar Oscar X Zakazakazi Zakazakazi amlipua Oscar Oscar

Sat, 1 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuzungumzwa kwa muda mrefu mtindo ambao Maofisa habari wa Vilabu vya Soka nchini wanafanya kazi hiyo kinyume na weledi, Hatimaye Afisa habari wa Azam FC, Thabit Zakaria "Zakazakazi" ameamua kutoa somo kuhusu suala hilo.

Zakazakazi ameamua kuvunja ukimya huo baada ya mchambuzi mahiri wa Soka, Oscar Oscar kuibua mjadala huo kwa mara nyingine katika kipindi cha michezo cha "Number Ten" kinachorushwa na TV E, akisema Maofisa wa Vilabu vya Soka nchini wanafanya majukumu zaidi ya kuhabarisha wapenzi, mashabiki wa Vilabu hivyo.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagrama Zaka ameandika ujumbe huu kwa Oscar Oscar:

"KWAKO BABA MZUNGU

Kuiga siyo kitu kibaya, lakini unatakiwa uwe makini kwenye uigaji wako.

Kuna copy and paste na kuna copy, customize and paste.

Yanayofanyika Ulaya hatuwezi kuyachukua na kuyatumia kama yalivyo (copy and paste), bali tunaweza kuyachukua, kuyaweka kwenye mazingira yetu na kuyatumia (copy, customize and paste).

Baba mzungu, heshimu sana mazingira ya kila watu na maeneo yao. Mazingira ninayoyasema hapa siyo misitu, ni utamaduni, mazoea, historia ya maisha, utendaji na uendeshaji wa mambo.

Kila watu katika maeneo yao wana tamaduni zao, historia zao na namna zao za utendaji wa mambo yao.

Ndiyo maana ligi kuu ya soka ya Marekani, MLS, timu hazishuki daraja wala hazipandi...huo ndiyo utamaduni wa michezo yote ya Marekani!

Ulaya hutumia maafisa habari bubu, yaani afisa habari aliyefungwa mdomo...hasemi chochote. Anachofanya ndiyo hicho unachokizungumza hapo...huo ni utamaduni wao, siyo kanuni wala sheria.

Kwa mazingira ya Tanzania hatuwezi kuwa afisa habari bubu kama Ulaya.

Klabu inaweka taarifa kwenye tovuti au kurasa rasmi za mitandao ya kijamii, bado vyombo vya habari vitataka sauti ya afisa habari, kwamba ile taarifa pekee haitoshi...ndiyo utamaduni wetu.

Utapigiwa simu na redio kutoka kila kona ya nchi, 'tumeona taarifa kwenye ukurasa wenu wa Instagram, hiyo taarifa ina ukweli kiasi gani?

Au imefanyika press conference kuelekea mechi...kaongea kocha na mchezaji mmoja, lakini bado waandishi watakupigia kutaka useme kitu.

Usiposema chochote, kuna ndugu mchambuzi mmoja hapo hapo ataanza kukuchambia wewe kwamba huna ushirikiano na vyombo vya habari, hivyo huna weledi.

Unageuka mjadala, na kwa sababu wewe haupo kujitetea kwamba unafanya kama Ulaya, basi wanabaki peke yao, wanakupiga za uso tu!

Watu wa Ulaya wanafanya mambo yao kutokana na mazingira yao, na sisi tunafanya mambo yetu kutokana na mazingira yetu.

Siyo kila kinachofaa Ulaya, kinafaa kila sehemu... hapana.

Copy, customize and paste!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live