Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zakazakazi: Kwa nini Prince Dube na fei Toto hawamo kwenye Tuzo?

Nzengeli Baleke Fei Toto Maxi, Baleke, Fei Toto.

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Azam, Zakaria Thabiti 'Zakazakazi' amesema kuwa kiungo wa Klabu hiyo, Feisal Salum 'Fei Toto' na mshambuliaji wao, Prince Dube walipaswa kuwa kwenye kinyang'anyiro cha Mchezaji Bora wa Ligi badala ya kumweka mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke.

Katika tuzo hizo zilizotangazwa jana na Bodi ya Ligi, kiungo wa Yanga, Maxi Mpia Nzengeli raia wa Congo DR alishinda tuzo ya mchezaji Bora wa mwezi Agosti wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara huku kocha wake, Miguel Angel Gamondi akishinda tuzo ya kocha bora wa mwezi.

Nzengeli amecheza mechi mbili za Ligi mwezi Agosti na kufanikiwa kufunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao wakati klabu yake ikishinda mabao 10 katika mechi hizo mbili na kukaa kileleni mwa ligi ikiwa na alama 6.

Ameandika Zakazakazi;

"Huwa wanazingatia nini? Maxi Nzengeli ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu, kwa mwezi Agosti. Hongera sana kwake, amekuwa na kiwango kizuri sana! Amewashinda Aziz na Jean Baleke ambao aliingia nao fainali, hongera sana kwao pia, wamekuwa na viwango vizuri sana!

"Lakini, ni vigezo gani hutumika kuteua hawa wachezaji? Ni hizi hizi takwimu tunazoziona kwenye taarifa rasmi za mamlaka, au kuna vigezo vingine ambavyo huwa havitajwi?

"Kwa sababu, takwimu za mshindi, Maxi Nzengeli, zinafanana na za Prince Dube;

Maxi Nzengeli

-Mechi 2

-Mabao 2

-Assist 1

Prince Dube

-Mechi 2

-Mabao 2

-Assist 1

Kwanini Prince Dube hayupo kwenye fainali?

Walioingia fainali

Aziz Ki

-Mechi 2

-Mabao 2

-Assist 1

Jean Baleke

-Mechi 2

-Mabao 2

-Assist 0

-Kadi ya njano 1.

"Yaani Baleke anaingiaje fainali halafu Dube hayumo? Katika hizi mechi mbili, Baleke ana kadi moja ya njano maana yake kwenye nidhamu alikuwa chini kidogo!

"Mbaya zaidi, Feisal Salum ana mabao 3 kwenye mechi hizi mbili, mengi kuliko wote hao, nakosaje kuingia fainali?

Vigezo gani vimetumika kumuweka Baleke mwenye mabao mawili bila assist, juu ya Feisal mwenye mabao 3?," amesema Zakazakazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: