Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zakazakazi: Hongera Ally Kamwe umekuwa Afisa Habari kamili

Ally  Kamwe X Malogo Ally Kamwe na mwamuzi Tatu Malogo

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe kupigwa adhabu kwa kosa la kumdhalilisha mwamuzi wa mchezo wa Singida dhidi ya Simba.

Mkuu wa Kitengo cha Habari Azam FC, Thabit Zakaria "zakazakazi" amempongeza Ally Kamwe na kuandika ujumbe huu;

Wakati Frank Lampard anafukuzwa na Chelsea kama kocha, Jose Mourinho alimpigia simu na kumwambia, 'Hongera sana, sasa ndiyo umekuwa kocha kamili '.

Mourinho alimaanisha kazi ya ukocha na kufukuzwa ni pacha, ndiyo maana wenyewe wanasema makocha huajiriwa ili wafukuzwe.

Na mimi napenda kutumia mfano huo kukupongeza mdogo. Hongera sana, sasa ndiyo umekuwa afisa habari kamili.

Hii kazi ya kuisemea timu kwenye mazingira kama ya nchi yetu, ni vigumu sana kuepuka hizi ajali ndogondogo za kuteleza ulimi au kidole.

Tunapitia magumu mengi sana ambayo huelekezwa kwetu na watu wanaoshindwa kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja.

Binadamu tumeumbwa na hisia ambazo huitwa majina tofauti kutokana na wakati na mazingira.

Wakati mpira umeisha katika mazingira ya kutotendewa haki, hisia hizi huitwa HASIRA.

Unapokuwa na hasira uwezo wa kujidhibiti hupungua sana. Sasa hapo ndiyo wanakuja waandishi na vinasa sauti vyao..hatari!

Au kama utapona kwenye mtego huo kuna mtego wa mitandao ya kijamii.

Unaangalia kwenye makundi zogozi watu wanasema mmeonewa. Unaenda mjini Instagram watu wanasema mmeonewa. Huko kwa X nako hali kadhalika.

Unawezaje kujizuia? Unashika simu yako na wewe unaweka maneno...halafu ndiyo yanatokea haya.

Ndiyo nasema hizi ajali za kawaida, sawa na mchezaji kupewa kadi nyekundu...kawaida tu!

Lakini mi nadhani sasa ifikie wakati waamuzi nao wahojiwe na waandishi wa habari baada ya mchezo ili kuelezea hali ilivyokuwa uwanjani.

Mpira ukiisha apewe muda wa kwenda kuangalia video ya mechi kwa yale matukio tata ili ajiridhishe.

Halafu aje ajibu maswali ya waandishi, na kama alikosea basi aombe radhi.

Angalau hii itasiadia kupoza nyoyo za walioumizwa na makosa yake.

Huku kuomba omba radhi kutawasumbua maana kunawashusha sana mbele ya jamii.

Lakini kwa wale ambao hawakutendewa haki, kuombwa radhi kuna maana kubwa sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: