Wakati Klabu ya Polisi Tanzania inamchukua Kocha Mkuu Mwinyi Zahera malengo makubwa waliyojiwekea kwa pande zote mbili ni kuinusuru Klabu hiyo kubaki Ligi Kuu,Mpaka sasa shughuli imekua ngumu kwa Zahera na vijana wake kwa ujumla.
Polisi Tanzania wamekua na muendelezo mbaya sana katika Ligi huku wakibakiwa na michezo 4 katika Ligi,kwa sasa wapo nafasi ya 16 (mwisho) wakiwa na alama 19.
Michezo minne ambayo wamebakiwa nayo Polisi Tanzania katika Ligi Kuu.
Vs Ihefu (Nyumbani).
Vs Mtibwa Sugar (Nyumbani ).
Vs Simba Sc (Ugenini).
Vs Azam Fc (Ugenini).
Je, Papa ataweza kuokoa jahazi na kuibakisha Polisi Tanzania Ligi Kuu?