Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera kupewa majukumu haya Simba

Zahera Pic Data Zahera kupewa majukumu haya Simba

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KOCHA wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera yupo hapa nchini akiendelea na majukumu yake mapya kimya kimya tangu alivyondoka katika kikosi cha Gwambina ya Mwanza msimu huu.

Zahera baada ya kumalizana na Yanga alikuwa Mkurugenzi wa ufundi katika kikosi cha Gwambina kabla ya kuachana na kibarua hicho kisha kutua Simba kimya kimya.

Mkongomani huyo baada ya kutua Simba wamekubaliana kuwa anafanya kazi ndani ya kikosi hicho kimya kimya na akiendelea kutimiza majukumu yake sita bila kufahamika mahala popote.

Mwanaspoti ambalo lilikufichulia Zahera kujiunga na Simba na wengine wakafuata limepata taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba kuwa, amepewa majukumu sita ya kuyafanya.

Taarifa hiyo inaeleza jukumu ya kwanza ambalo analifanya Zahera anatakiwa kuvumbua vipaji kwa ajili ya timu zote tatu ile ya vijana, wanawake na wakubwa.

Kazi hiyo ya kugundua vipaji wanatakiwa kuwa ndani au nje ya nchi lakini amepewa jukumu la kuisimamia timu ya vijana katika masuala ya kiufundi.

"Zahera anatakiwa kuwa sehemu ya mikakati ya timu yetu katika masuala ya kiufundi pamoja na maendeleo kwa kushauri au kutoa ambalo analifahamu," alisema mtoa taarifa huyo na kuongezea;

"Kuanzia sasa anatakiwa kuwa mshauri katika masuala ya usajili kwa wachezaji wenye uwezo wa kuisaidia Simba kutokana na mapungufu ambayo wameyaonyesha awe mchezaji wa ndani au nje ya nchi.

"Amekuwa akishauri masuala muhimu katika benchi la ufundi ambalo lipo chini ya kocha wetu, Didier GomesĀ  na amekuwa akiangalia masuala ya kimaendeleo ndani na nje ya timu."

Hata hivyo, uongozi wa Simba haukukiri moja kwa moja kama wamempa ajira kocha huyo ingawa wamesema wamepokea maombi ya makocha wanne kwa ajili ya timu ya vijana.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again' amesema kwasasa hakuna mchakato kuhusu Zahera lakini kama mipango yao ya kumsaka kocha wa vijana ikikamilika basi wataweka wazi.

"Kuhusu Zahera sio kweli, ila tuko kwenye mpango wa kusaka kocha kwa ajili ya timu ya vijana, tukimaliza tutaweka wazi maana sio mchakato wenye presha bali tunakwenda nao taratibu tu.

"Kama atakuwa Zahera ama mwingine basi hapo baadaye itakuwa wazi na sio sasa hivi," amesema Try Again

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz