Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera kumrudisha Ajibu wa Yanga?

Drg Ajibu Zahera kumrudisha Ajibu wa Yanga?

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mwinyi Zahera ameendelea kukijenga kikosi cha Coastal Union ili kuleta ushindani kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu huku mwenyewe akitamba kurejesha ubora wa wachezaji wake akiwemo staa wa zamani wa Simba, Yanga, Azam na Singida Big Star, Ibrahim Ajibu.

Zahera anaamini kwenye kipaji cha Ajibu na alivyopewa mikoba ya kuinoa Coastal tu, akamsajili kiungo huyo ambaye waliwahi kufanya kazi kwa pamoja wakiwa Yanga msimu wa 2017/2018 ambao Ajibu alikuwa kwenye kiwango bora akimaliza ligi na mabao sita na asisti 17 kisha msimu uliofuata akasajiliwa na Simba.

Baada ya hapo kiwango cha Ajibu kimekuwa cha kusuasua kwani hata alivyoenda Simba hakuonyesha ubora kama alivyofanya msimu wa 2017/18 na mwisho wa siku klabu hiyo ikaachana naye na kutua Azam ambako nako hali haikuwa nzuri kisha Singida na sasa Coastal.

Licha ya kuishia kukaa benchi kwenye mechi ya kwanza ambayo walipoteza kwa kufungwa 2-1 na Dodoma Jiji, Ajibu alianzishwa mechi ya pili ya Coastal iliyopigwa juzi Jumapili ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar na kuifungia timu hiyo bao la kuongoza dakika ya 71 kabla ya Mtibwa kusawazisha dakika ya 84 kupitia Kassim Haruna.

Akizungumza nasi, Zahera ambaye ni raia wa DR Congo alikiri kumkubali Ajibu; “ kutokana na kipaji chake na kusema anataka kumfanya awe bora zaidi kama ilivyokuwa msimu wa 2017/18.

“Ni mchezaji mzuri na namkubali, tunatengeneza timu kupitia mchezaji mmoja mmoja hivyo Ajibu ni miongoni mwao, nataka arejee kwenye ubora wake na naamini msimu huu atafanya hivyo,” alisema Zahera aliyempa unahodha Ajibu ndani ya Coastal kama ilivyokuwa kwa Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live