Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera kazi nzito Polisi Tanzania

Polisi Tz XZahera.jpeg Mwinyi Zahera akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Polisi

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabosi wa Polisi Tanzania wamepania kurudi kwa kishindo mzunguko huu wa pili wa Ligi Kuu Bara baada ya kuanza vibaya, huko kocha wao akianza kukuna kichwa kwa ajili ya kukiboresha kikosi hicho kupitia dirisha dogo lililofunguliwa rasmi.

Mabosi hao wamedhamiria kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja ambapo jambo la kwanza ni kupitia ripoti ya kocha wao, Mwinyi Zahera, kwa ajili ya maboresho ya kikosi chao na lingine ni kuongeza posho za wachezaji kwa kila mechi.

Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Robert Munisi, alisema kwa sasa wameandaa mikakati mizuri ya kuhakikisha hali waliyonayo wanaondokana nayo kwa kuweka misingi imara na rafiki kwa wachezaji ikiwa ni sehemu ya motisha.

“Yapo maeneo mengi yaliyotuangusha katika mzunguko wa kwanza ila sisi viongozi tumekaa chini na kuona ni kwa kiasi gani tunaweza kuondoa hili ili tuweze kufanya vizuri na kutoka mkiani,” alisema na kuongeza;

“Mikakati tunayoifikiria ni kuongeza bonasi za wachezaji wetu kwenye kila mchezo na wakati huo tunaangalia nyota wapya watakaotusaidia katika dirisha hili dogo kutokana na ripoti iliyowekwa mezani na kocha wetu.”

Katika mzunguko wa kwanza kikosi hicho kimeshinda michezo miwili tu, sare mitatu na kupoteza 10, kikisalia mkiani na pointi tisa huku kikikabiliwa na mechi ngumu kesho Jumamosi dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Polisi ilimchukua Kocha Zahera aliyewahi kuinoa Yanga kumpa nafasi ya kocha mkuu na tayari ameanza mikakati ya kukabiliana na waajiriwa wake hao wa zamani, sambamba na kusaka mashine mpya za kuimarisha kikosi hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live