Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera aweka sawa ishu ya Ajibu

49353 Yanga+pic

Fri, 29 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIKOSI cha Yanga kimetua jijini Mwanza jana asubuhi kwa ajili ya kuwinda ushindi mbele ya Alliance kwenye mchezo wa robo fainali wa Kombe la FA, huku Kocha Mwinyi Zahera akiweka sawa ishu ya nahodha wake, Ibrahim Ajibu. Yanga imetua jana asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kupokewa na mamia ya mashabiki wake na jioni wakafanya mazoezi ikiwa ni mikakati ya Zahera kuhakikisha wanashinda na kusonga mbele hatua ya nusu fainali na baadaye fainali.

Hata hivyo, mchezo huo utakapigwa kwenye dimba la CCM Kirumba jinni hapa, unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhitaji ushindi ili kusonga mbele.

Lakini, Zahera na jeshi lake litaingia uwanjani wakiwa na rekodi ya nzuri msimu huu baada ya kushinda mechi mbili za Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC na Alliance uwanjani hapo ikiwa ni rekodi mpya. Yanga kwa misimu miwili haikuwa imepata ushindi wowote katika mechi tatu ilizocheza na Mbao FC, lakini chini ya Zahera mambo yamekuwa tofauti na kushinda mechi zote.

Ugumu wa mchezo wa Jumamosi ni kwamba, Yanga itataka kuendeleza rekodi huku Alliance wakijipanga kulipiza kisasi na kusonga mbele. Mara baada ya kutua mjini hapa, Zahera akalieleza Mwanaspoti kuwa mchezo huo ni muhimu kwa timu yake na kwamba, malengo ni kushinda na kusonga mbele licha ya kufahamu wapinzani wake ni washindani wazuri.

“Hatuwezi kuwa na mpango mwingine tofauti na ushindi, utakuwa ni mchezo mzuri kwa timu zote, tumekuja kutafuta nafasi ya kusonga mbele hadi kucheza fainali,” alisema Zahera.

Ajibu nje

Kuhusu Ajibu, Zahera alisema kuwa hatakuwepo kwenye mchezo huo lakini, kila kitu kitakuwa sawa na waliopo kikosini watafanya majukumu yao kikamilifu.

Alisema kuwa Ajibu hakuambatana na timu kutokana na kutofanya mazoezi na wenzake kwa muda mrefu kwa kuwa, hakuwa vizuri kiafya. “Ajibu alianza mazoezi juzi hivyo hawezi kuwa miongoni mwa wachezaji watakaocheza Jumamosi, lakini timu itaendelea kuwa imara na waliokuwepo watatimiza malengo,” alisema.

mechi ya Lipuli

Mkongomani huyo alisema kuwa pamoja na kupoteza mchezo dhidi ya Lipuli, lakini kikosi chake kilicheza vizuri na wapinzani walipata nafasi moja wakaitumia vyema.

“Hakuna makosa waliyoyafanya, Yanga walipata nafasi nyingi kuliko Lipuli ambao, walipiga shuti moja lililozaa bao, ila vijana wangu walipambana,” alisema.



Chanzo: mwananchi.co.tz