Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera auma meno Polisi Tanzania

Zahera Pic Papaaaa Mwinyi Zahera bado anahaha kuweka mambo sawa Polisi Tanzania

Sun, 25 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kushindwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi tatu mfululizo tangu ameachiwa timu Kocha wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera ameuma meno, huku akikiri mambo ni magumu.

Polisi inaburuza mkia ikiwa imecheza mechi 17 imekusanya pointi tisa.

Zahera alisema uongozi wa timu hiyo unatakiwa kuwezeka kwenye usajili dirisha hili kwa kuwaongeza wachezaji wenye ubora ili wairudishe timu kwenye ushindani.

“Kazi yangu kama kocha nimeshaikamilisha mapema kwa kuwapa ripoti ni maeneo gani yanatakiwa kuongezewa nguvu kilichobaki ni utekelezaji na nimeongea na viongozi kuwasisitiza kuwa kama wanataka kuona timu inaendelea kushiriki Ligi Kuu wazingatie mahitaji,” alisema na kuongeza;

“Kwenye maeneo ni timu nzima imepwaya kuanzia kipa hadi washambuliaji, uongozi unalifahamu hilo tusubiri kuona ni nafasi gani nilizopendekezwa zitafanyiwa kazi ili kuweza kuipambania timu iweze kubaki.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live