Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera asaka mechi za kirafiki Dar

Mwinyi Zahera Namungo Kocha Mkuu wa Namungo FC, Mwinyi Zahera

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Namungo FC, Mwinyi Zahera, ambaye timu yake imeweka kambi Dar es salaam, amesema anahitaji kupata mechi mbalimbali za kirafiki ili kuwaimarisha wachezaji wake kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara kurejea baadae mwezi ujao.

Namungo yenye maskani yake Ruangwa, Lindi inafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Bandari uliopo Temeke, jijini humo.

Zahera, amesema anaamini watatumia kwa umakini muda uliopo kurekebisha mapungufu aliyoyabaini, ili kurejea katika ligi wakiwa imara.

Zahera amesema anafahamu Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa ina ushindani mkubwa na utaongezeka kuingia katika duru la pili ambalo kila timu inahitaji kufikia malengo iliyojiwekea.

“Tumerejea mazoezini kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mechi zilizopita, lakini pia muhimu kutengeneza muunganiko wa wachezaji waliosajiliwa dirisha dogo na wale walikukuwepo awali.

Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwa sababu tunaamini tutafanya vizuri, kazi iliyoko mbele yetu ni kupanbana katika kila mechi tutakayocheza,” amesema Zahera.

Young Africans ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Azam FC ndio vinara wa ligi hiyo yenye timu 16.

Chanzo: Dar24