Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera apewa rungu hili Polisi Tanzania

Zahera Pic Papaaaa Zahera apewa rungu hili Polisi Tanzania

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mpya wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera, ameanza vibaya kibarua chake katika kikosi hicho cha Maafande baada ya kufungwa bao 1-0 na Azam FC, juzi Jumatatu katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Zahera aliyewahi kuifundisha Yanga huku akiwahi pia kuwa Mkurugenzi wa Soka la Vijana na Wanawake, aliteuliwa kukiongoza kikosi hicho Desemba 2, kufuatia kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha Mkuu, Mrundi Joslin Bipfubusa, Oktoba 26.

Akizungumza Makamu Mwenyekiti wa Klabu wa Polisi Tanzania, Robert Munis alisema wana imani kubwa na Zahera huku wakiamini licha ya kuanza vibaya bado ana uwezo wa kuwatoa mkiani na kuwarejesha katika nafasi za juu.

“Tumempa uhuru wa kuangalia ni maeneo gani anaona kuna upungufu ili katika dirisha hili litakalofunguliwa hivi karibuni tumtimizie mahitaji yake, tunaamini mzunguko wa pili tutafanya vizuri,” alisema Munis na kuongeza;

“Tulikuwa na matumaini makubwa sana ya kufanya vizuri kabla ya msimu kuanza lakini kwa bahati mbaya tunaona tunazidi kutoka nje ya malengo jambo ambalo tunataka kulifanyia kazi haraka ili kuokoa hali inayoendelea,” alimalizia kiongozi huyo.

Baada ya Joslin kuondoka kikosi hicho kilikuwa chini ya kocha wa viungo John Tamba ambaye alikiongoza kwenye michezo sita ya Ligi Kuu ambapo kati ya michezo hiyo alishinda mmoja tu kwa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu Novemba 17, sare mmoja na kupoteza michezo minne.

Chanzo: Mwanaspoti