Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera apangua idara zote Yanga ikivaa Polisi

78334 Yangaaa+pic

Thu, 3 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera atakuwa akiiongoza timu yake kwa macho jukwaani, amefanya mabadiliko kadhaa katika kikosi chake kitakachoanza katika mchezo huo leo dhidi ya Polisi Tanzania.

Zahera amepangua safu ya ulinzi ya Yanga akimuanzisha kwa mara ya kwanza nahodha wake msaidizi Juma Abdul katika beki ya kulia akichukua nafasi ya Ally Ally alianzia benchi.

Mbali na Abdul golini Yanga ameendelea kuwa kipa mzawa Metacha Mnata, beki wa kushoto akiwa Ally Mtoni 'Sonso' akiendelea kucheza na mabeki wa kati Lamine Moro na Kelvin Yondani.

Safu ya kiungo Yanga itakuwa chini ya viungo wawili Wazanzibar Abdulaziz Makame na Feisal Salum 'Fei Toto huku ingizo jipya akiwa winga mkongwe Mrisho Ngassa anayeingia kuchukua nafasi ya Patrick Sibomana ambaye ni majeruhi.

Katika safu ya ushambuliaji Yanga itamkosa nahodha wao Papy Tshishimbi ambaye inaelezwa kuwa ni majeruhi ambapo Juma Balinya ameingia kuchukua nafasi yake akicheza sambamba na David Molinga ambaye naye ameingia katika kikosi cha sambamba wakicheza sambamba na Sadney Urikhob.

Katika benchi kipa Farouk Shikhalo ameendelea kuwa benchiĀ  sambamba na mabeki Ally,Mustapha Seleman,Mharami Issa 'Marcelo',viungo wakiwa Deuse Kaseke,Jafary Mohamed,Deuse Kaseke na Mapinduzi Balama ambaye amerejea kutoka majeruhi.

Pia Soma

Advertisement

Yanga inaingia katika mchezo huo ikisaka ushindi au sare ya kwanza tangu kuanza kwa ligi baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting huku kocha wao Zahera akiwa jukwaani akitumikia adhabu ya kusimamishwa mechi tatu kwa makosa ya matamshi makali baada ya kipigo cha kwanza iliyotolewa na kamati ya usimamizi wa ligi.

Yanga itakuwa chini ya makocha wawili wasaidizi Noel Mwandila na Peter Manyika lakini pia wakiwa na lengo la kutaka kulipa kisasi baada ya Polisi kuwachapa mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki kwa kujipima nguvu uliopigwa Agosti 16 mjiniĀ  Moshi.

Chanzo: mwananchi.co.tz