Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera acharuka afanya mabadiliko mawili Zambia

77659 Zahera+pic

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefanya mabadiliko mawili katika kikosi chake kitakachoshuka Uwanja wa Levy Mwanawasa,mjini Ndola, Zambia leo Jumamosi kukabiliana na wenyeji wao Zesco.

Katika kikosi kilichotangazwa muda huu Zahera katika ukuta ameanza na kipa Metacha Mnata, Ally Ally aliyeingia kikosi cha kwanza kuchukua nafasi ya Mapinduzi Balama aliyeumia mchezo wa kwanza huku mabeki wengine wakiwa Ally Mtoni 'Sonso',Lamine Moro na Kelvin Yondani.

Nafasi ya kiungo amemuweka jukwaani Mohamed Issa 'Banka' anayetajwa kupata maumivu nafasi yake kuchukuliwa na Deus Kaseke.

Sambamba na Kaseke viungo wengine ni Feisal Salum 'Fei Toto', Abdulaziz Makame na Patrick Sibomana.

Safu ya ushambuliaji Zahera amewaacha nahodha Papy Tshishimbi na Sydney Urikhob kama ambavyo walicheza mchezo wa kwanza.

Katika benchi Zahera amewapa nafasi kipa Mkenya Farouk Shikhalo, Muharami Issa, Juma Abdul, Mrisho Ngassa, Juma Balinya, Maybin Kalengo na Jafary Mohamed.

Yanga baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 wakiwa nyumbani wiki mbili zilizopita wanahitaji ushindi wa sare ya kuanzia mabao mawili waweze kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chanzo: mwananchi.co.tz