Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera aanza kazi na masharti mazito

Mwinyi Zahera Atimuliwa Mwinyi Zahera

Mon, 1 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Namungo imefikia makubaliano na Kocha, Mwinyi Zahera kwa ajili ya kukiongoza kikosi hicho msimu huu huku akitoa masharti kwa viongozi kumuachia suala nzima la usajili wa timu hiyo kwenye dirisha hili dogo.

Mmoja wa kiongozi wa Namungo (jina tunalo) aliliambia Mwanaspoti wakati wanamfuata kocha huyo kwa ajili ya mazungumzo ya kukiongoza kikosi hicho aliwaambia kama wamedhamiria kumpata basi waache afanye maamuzi yote ya timu atakayoona yanafaa.

“Sisi kama viongozi wenye weledi na kuheshimu taaluma za watu alivyotuambia hivyo tuliona hakuna shida yoyote ndio maana tukafikia makubaliano hayo, tunaamini ni kocha mzuri atakayetufikisha mbali zaidi ya hapa,” alisema mmoja wa kiongozi.

Kwa upande wa Zahera alisema ni furaha kwake kuaminiwa na kupewa nafasi hiyo huku akiwaomba zaidi ushirikiano viongozi na wachezaji ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea ikiwemo la kumaliza nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu.

Zahera aliyekuwa Kocha Mkuu wa Coastal Union msimu huu kisha kuhamishiwa kwenye Ukurugenzi wa Programu za Soka la vijana katika kikosi hicho ameondoka na kutimkia Namungo baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kuongezewa mkataba mwingine.

Mkataba wa Zahera na Coastal umefikia tamati leo Desemba 31 na ameenda Namungo kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Denis Kitambi aliyetimkia Geita Gold baada ya kuiongoza timu hiyo kufuatia Mrundi, Cedric Kaze kuondoka Oktoba 22, mwaka huu.

Chanzo: Mwanaspoti