Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zahera: Yanga, Simba zisitarajie mteremko

Gwambina+pic Zahera: Yanga, Simba zisitarajie mteremko

Wed, 19 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Saddam SadickMKURUGENZI wa benchi la ufundi la Gwambina FC, Mwinyi Zahera amesema sababu iliyomvutia kujiunga na timu hiyo ni kutokana na mipango endelevu aliyoikuta kwa uongozi na kwamba malengo yake itakuwa ni kuwania taji kila msimu.

Zahera alitemwa na Yanga katikati ya msimu uliopita ambapo kwa sasa analiongoza benchi la ufundi la Gwambina likiongozwa na Kocha Mkuu, Fulgence Novatus na Athuman Bilali 'Billo'.

Akizungumza leo Agosti 19, 2020 wakati wa utambulisho, Zahera amesema aliamua kujiunga na timu hiyo baada ya kuridhika na mikakati iliyonayo klabu kwa maendeleo endelevu ikiwamo soka la vijana.

Amesema kutokana na uwezo na uzoefu alionao katika soka la ushindani katika nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania, anaamini timu hiyo itatesa sana na itakuwa yenye kugombea mataji kila msimu na kwamba hiyo ndio falsafa yake.

"Mimi timu yoyote Afrika hata Ulaya naweza kufanya nayo kazi kama nitaridhika na mipango ya uongozi, kwahiyo nimekuja Gwambina kuhakikisha nafanya makubwa ambayo hawatajutia" amesema Zahera.

Kocha huyo ameongeza kuwa licha ya Gwambina kuwa msimu wake wa kwanza kushiriki Ligi Kuu, lakini haoni kipya kwani hata Simba, Yanga na Azam wasitarajie mteremko kwani Ligi haina mwenyewe isipokuwa maandalizi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz