Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zaha anunua Timu

Zaha And Stormy.png Zaha anunua Timu

Fri, 30 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa soka, Wilfried Zaha na rapa Stormzy wametangaza mpango wao wa kuinunua timu ya Croydon Athletic.

Winga, Zaha, anayemaliza mkataba wake huko Crystal Palace ameungana na rapa wa Uingereza, Stormzy kama sehemu ya watu watatu watakaoinunua klabu hiyo ya soka, Croydon Athletic.

Kilichoelezwa ni kwamba kwa muda mrefu wawili hao wamekuwa kwenye mchakato wa kuimiliki timu hiyo. Taarifa yao ilibainisha: “Tunafurahia kutangaza zama mpya za AFC Croydon Athletic, imebaki kwenye uthibitisho wa mwisho wa kutoka FA na ligi. Huu ni mjadala uliochukua miezi mingi ya majadiliano.”

Klabu hiyo ya Croydon Athletic FC iliyoanzishwa 2012 inacheza Ligi Daraja la Tisa huko England.

Inamiliki uwanja wenye uwezo wa kuingiza watazamaji wanaoketi 3,000 ambao unaitwa Maryfield.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live