Bodi inayosimamia Ligi kuu ya Zanzibar (PBZ) imepitisha kanuni mpya za Usajili kuwa Klabu yoyote itakayomsaini mchezaji kutoka Tanzania bara ataingizwa kwenye system kama Mchezaji wa kigeni kwa maana lazima akatiwe Kibali cha kuishi Zanzibar ambacho kina gharimu pesa za kitanzania laki 5.
Pia kwenye klabu Moja hawatakiwi kuzidi wachezaji 9
Kwa ligi ngazi ya Mkoa Mvhezaji kutoka Tanzania bara atakatiwa kibali cha kuishi na kufanya kazi kwa msimu. Mmoja ambacho kita gharimu Pesa za kitanzania Laki 3.
Kwa upande wa Tanzania Bara, mchezaji akisajiliwa kutoka Zanzibar anahesabika ni mzawa.
Je hii inatengeneza Usawa wa ajira ama Ubaguzi wa Ajira ? Au lengo ni nini ?
Hii kitaalamu inakuwaje kwa kanuni mpya hizo kwa msimu huu wa 23/24 zimeanza kazi.
Tupe maoni yako