Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ZANDANI KABISA: Nabi afungashiwa virago Yanga

Nabi Byebye ZANDANI KABISA: Nabi afungashiwa virago Yanga

Tue, 25 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ZA NDANI KABISA! Taarifa za kikachero kutoka ndani ya Klabu ya Yanga zinaeleza kuwa, uongozi wa Klabu hiyo umefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha wao mkuu Nasserdine Mohammed Nabi baada ya kocha huyo kutoifikisha timu hiyo hatua ya makundi katika mashindano ya klabu Bingwa Afrika 'CAFCL'.

Inaelezwa kuwa, Kocha Nabi alivyosaini kanadarasi mpya ndani ya Timu hiyo makubaliano makuu na viongozi wa Yanga ilikuwa ni kuifikisha timu hiyo hatua ya makundi 'CAFCL' pamoja nakutetea vikombe vyote walivyoweza kuvishinda msimu uliopita.

Huku Msaidizi wake Cedric Kaze atabadilishiwa majukumu na kwenda kuchukua nafasi ya Mwinyi Zahera kusimamia Soka la Vijana (Yanga U17, U20 na Yanga Princess).

Taarifa rasmi ya klabu hiyo kuvunja mkataba na kocha huyo raia wa Tunisia inatarajiwa kutolewa rasmi na uongozi wa klabu hiyo wakati wowote kuanzia sasa.

Kocha Nabi ambaye alianza kuwatumikia Wananchi hao wa Jangwani Aprili 2021, amecheza mechi za Ligi 43 bila kupoteza, Mshindi wa Ligi Kuu, Mshindi wa FA, Ngao ya Jamii mara 2 huku akiondolewa katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Al Hilal ya SUda.

"Nabi akifukuzwa Yanga atapata timu haraka kuliko kocha yoyote ndani ya Tanzania, inaweza ikatolewa press release (Taarifa kwa vyombo vya habari) huku kesho akatambulishwa huku na mimi binafsi sitoshangaa kama Nabi atapata nafasi Simba au Azam "- Farhan.

"Nabi bado kocha wa Yanga na hapa Yanga wamepita watu wengi, alikuwepo Tabu Mangala hivyo hata akiondoka bado hakuna kitu cha kushangaza" Alex Ngai Mjumbe wa kamati ya utendaji Yanga akizungumza kwenye Sports HQ ya EFM.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live