Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ZA NDANI KABISA: Phiri amesinya miwili Msimbazi

Phiri Simba Ml Moses Phiri

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya klabu ya Simba zinaeleza kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Moses Phiri (27) amejiunga na miamba hiyo ya Msimbazi.

Nyota huyo wa Klabu ya Zanaco ya Zambia amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Simba SC na anatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Phiri ambaye alikuwa mfungaji Bora wa ligi kuu ya Zambia msimu wa 2020/2021 akiwa na magoli 13.

Inaelezwa kuwa, Phiri anakwenda kuchukua nafasi ya Mkongomani, Chris Mushimba Mugalu (31) ambaye anadaiwa Simba itaachana naye kutokana kiwango chake kutoridhisha msimu huu unaomaliza.

Wachezaji wanaowindwa na Simba mpaka sasa 1. Ceasar Manzoki - Straika 2. George Mpole - Straika 3. Morlaye Sylla - Kiungo DONE DEAL 1. Moses Phiri - Straika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live