Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yusuph Bakhresa awatega wachezaji Azam FC

Image 376.png Yusuph Bakhresa awatega wachezaji Azam FC

Thu, 11 May 2023 Chanzo: Dar24

Wachezaji wa Azam FC wana nafasi kubwa ya kuweka kambi Barani Ulaya wakati wa maandalizi ya msimu ujao wa 2023/24, endapo watafanikiwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ msimu huu 2022/23.

Azam FC imetinga Fainali ya Michuano hiyo kwa kuifunga Simba SC 2-1 katika mchezo wa Nusu Fainali uliopigwa Jumapili (Mei 07) katika Uwanja Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Afisa Habari wa Azam FC Hashim Ibwe amesema ahadi hiyo kwa Wachezaji imetolewa na Bosi wao Yusuph Bakhresa, huku nchi za Hispania, Ubelgiji au Sweden zikitajwa.

Ibwe amesema tayari tayari Bosi huyo amekamilisha mpango wake wa maandalizi ya msimu ujao kwa timu hiyo, lakini mtihani umebaki kwa wachezaji wa Azam FC kuhakikisha wanashindwa mchezo wa Fainali na kutwaa Ubingwa wa ASFC.

“Tunamshukuru sana Mungu kwa kutujaalia kuingia katika hatua hii ya Fainali maana haikuwa kazi rahisi, hivyo sasa lengo kubwa ni kutwaa ubingwa na kuanza maandalizi ya msimu ujao ambapo tajiri katuahidi kuweka kambi Ulaya.”

“Awali kambi yetu ilitakiwa twende Tunisia ila bosi kasema kama tutachukua ubingwa tutaenda kati ya Hispania, Ubelgiji au Sweden, mbali na hivyo, pia tunatarajia kufanya usajili wa kutisha ndiyo maana kocha mpya yupo nchini mapema,” amesema lbwe

Azam FC inasubiri mshindi wa mchezo wa Nusu Fainali ya pili ya ASFC kati ya Mabingwa watetezi Young Africans na Singida Big Stars itakayokua nyumbani katika Uwanja wa CCM Liti mjini Singida.

Chanzo: Dar24