Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yusuf Kagoma: Simba SC wajipange sana

Yusuph Kagoma Yusuf Kagoma

Mon, 7 Aug 2023 Chanzo: Dar24

Kiungo anayekipiga Singida Fountaine Gate, Yusuf Kagoma ameanza tambo mapema akisema timu hiyo ina kikosi bora na kuamini itafanya vizuri kimataifa, huku akisisita Tanga katika Ngao ya Jamii watakuwa na kazi moja tu kunyanyua kwapa.

Singida FG tayari imetangaza kikosi cha wachezaji 31 na imetua Tanga kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC Agosti 10.

Kagoma amesema baada ya mchezo dhidi ya AS Vita amekitathimini kikosi chao na kubaini uongozi umesajili wachezaji wenye uwezo kuanzia wanaokaa benchi hadi wanaoanza kikosi cha kwanza.

“Tuna timu nzuri ukiangalia waliokaa benchi siku ya mechi na AS Vita wana uwezo sawa na tulioanza, hivyo kazi iliyopo ni ushindani kwetu kusaka namba kikosi cha kwanza,” amesema Kagoma na kuongeza;

“Jambo lililofanywa na benchi la ufundi sambamba na uongozi ni kutuamsha wachezaji tuweze kuwa imara ili kupata namba ya kucheza kwa sababu ubora wa wachezaji na kujituma kwao kunaongeza changamoto.”

Akizungumzia mchezo dhidi ya Simba SC amesema; “Hautokuwa mchezo rahisi tumejiandaa kwa ajili ya kushinda japo hatutarajii mteremko tunajua kutokuwa na ushindani ila tunahitaji matokeo mazuri ili kutinga Fainali na baadae kutwaa taji.”

Chanzo: Dar24