Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yupo kimya eeh? Kishindo kinakuja

Banda Pic Data Yupo kimya eeh? Kishindo kinakuja

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

BEKI wa Kimataifa wa Tanzania, Abdi Banda ameeleza kuwa na nafasi kubwa ya kupata timu ya kuichezea msimu ujao wa Ligi Kuu Afrika Kusini.

Banda amesema hayo mara baada ya kurejea nchini akitokea Afrika Kusini ambako alikuwa akipambania nafasi ya kujiunga na Black Leopards lakini dili hilo lilitibuka mara baada ya kutimuliwa kwa Dylan Kerr.

Kerr alimpa mualiko Banda na kulikuwa na uwezekano kwa beki huyo wa zamani wa Simba na Coastal Union za Ligi Kuu Bara kupewa mkataba wakati wa dirisha dogo la usajili kabla ya Muingereza huyo kufutwa kazi.

“Wakati tukiwa na mipango hii, Mungu naye huwa na yake, haikuwa riziki kuichezea Black Leopards hivyo siwezi kusononeka, kuna sehemu nyingine nilijaribu kupambana lakini muda haukuwa rafiki sana upande wangu,”

“Naamini kila kitu hutokea kwa sababu kwa hizi wiki mbili tatu, nimeamua kwanza kurudi nyumbani ili nijipange upya kwa kufanya mazoezi ya hapa na pale kabla ya kurudi tena Afrika Kusini mwishoni mwa msimu,” alisema.

Akiongelea uwezekano wa kurudi nyumbani, Tanzania kucheza soka, Banda alisema kwa sasa bado anaamini kuwa ananguvu za kuendelea kushindani kwenye Ligi kubwa kama Afrika Kusini ambako amecheza kwa miaka minne.

“Sina mawazo kwa sasa ya kurudi nyumbani kucheza Ligi, napambana kusogea na sio kurudi nyuma, nikitoka Sauzi nitaenda kwingine ambako nitaona Ligi yao ipo juu ila kwa asilimia kubwa mipango yangu ipo sawa,” alisema.

Banda alianza kucheza soka Afrika Kusini akiwa na Baroka, 2017 ambayo aliichezea kwa miaka miwili halafu akaibukia Highlands Park.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz